Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Zaidi ya wachimbaji wadogo wa dhahabu 7000 wilayani Nzega mkoani
Tabora wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini kuwapatia
leseni ya uchimbaji katika mgodi mdogo wa dhahabu wa Mwanshina, uliopo
pembezoni mwa mgodi mkubwa wa dhahabu wa Resolute.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika mgodi
huo, waliomba Serikali iwapatie leseni hiyo licha ya kukiri kuvamia eneo
hilo kutokana na kukabiliwa na shida za kimaisha.
Walisema kuwa walivamia eneo hilo bila kuambiwa na kiongozi yeyote kutokana na ugumu wa maisha ya kukidhi haja zao za msing.
Mkazi wa Kijiji cha Mwanshina, JIsena Masanja
alisema walivamia eneo hilo lililopo pembezoni mwa mgodi mkubwa ambalo
halifanyiwi kazi na wawekezaji hao na kuongeza kuwa watalinda mazingira
ikiwamo kuimarisha usalama kwa wananchi.
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment