Home » » BASI LA AM COACH LAGONGANA NA ROLI

BASI LA AM COACH LAGONGANA NA ROLI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Ajali mbaya ya basi la kampuni ya AM Coach lenya namba T 763 AYN imetokea  mkoani Tabora baada ya basi hilo kugongana na lori mali ya kampuni ya soda ya Coca Cola lenye namba za usajili T 256 BPP

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa paparazi na mmoja wa abiria aliyenusurika kwenye ajali hiyo ni kama ifuatavyo:- 

"Dereva wa lori kajaribu kutukwepa lakini ufinyu wa barabara, mbele kuna lori scania linakuja,kwa hiyo akajikuta kagonga kushoto kwake na kulia kwake ila lori la kushoto kwetu halikusimama

Dereva wetu akashindwa kurudi upande wa kushoto kwa sababu kulikuwa na lori ambalo alikuwa anataka kulipita, basi letu lilikuwa 'linaovertake'(linataka kupita), basi nia AM Coach na lori ni la Coca Cola"

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa