Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Wilaya (DC) ya Igunga, Elibariki Kingu, amewakemea viongozi
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kijiji cha Igurubi kwa kumfukuza kazi
mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Selemani Mdeka, kwa madai ya
kutofautiana kwa kauli.
Viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Igurubi wanatokana na CCM na
uamuzi wa kumfukuza mwenyekiti wa serikali ya kijiji aliyechaguliwa na
wananchi umekifanya kijiji hicho kikose mwenyekiti wa kudumu kwa miezi
minne sasa na badala yake waliopo wanapokezana nafasi hiyo kulingana
na mahitaji ya wakati.
Hata hivyo, mwenyekiti aliyetimuliwa kwa matakwa ya chama anaendelea
na uanachama wake hali inayomfanya Ofisa Mtendaji Kata ya Igurubi
kukosa sababu za kuomba ruhusa ya kufanya uchaguzi mdogo wa kuziba
nafasi hiyo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment