Na Hastin Liumba, Sikonge
WILAYA ya Sikonge mkoani Tabora imedhamiria kuwakamata na kuwafungulia
mashitaka wazazi wote ambao wamewazuia au wameshindwa kuwaandikisha
watoto wao wenye umri wa kwenda shule.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa wilaya ya Sikonge Hanifa Selengu
alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Pangale katika hafla ya
uzinduzi wa mafunzo maalumu ya upandaji miti.
Alisema vitendo vya utoro wa wanafunzi vinavyozidi kushamiri katika
shule nyingi wilayani humo kwa kiasi kikubwa vinachangiwa na baadhi ya
wazazi ambao hawaelewi umuhimu wa elimu.
'Ili kukomesha tabia hii tutapita nyumba hadi nyumba kuwakamata wazazi
wote waliozuia watoto wao kwenda shule na kuwafungulia mashtaka.'
alisema Selengu.
Aidha alibainisha ni aibu kubwa kwa kata hiyo kuandikisha asilimia 65
tu ya watoto wote wenye umri wa kwenda shule huku wengine wakiacha
shule katikati ya safari kwa kisingizio cha kwenda kusaidia wazazi
kilimo cha tumbaku.
'Acheni kutumikisha watoto wenu katika mashamba ya tumbaku,
wapelekeni shule, wataendelea kuwategemea hadi lini, mtawafanya wawe
mbumbumbu kwa kutokujua kusoma na kuandika', aliongeza.
Akizungumzia hali hiyo diwani wa kata ya Pangale Hamis Mayilla
aliafiki hatua hiyo ya mkuu wa wilaya na kuongeza wamekuwa wakikemea
tabia ya baadhi ya wakulima katika kata hiyo kutopeleka watoto wao
shule.
Home »
» WAZAZI WASIOPELEKA WATOTO SHULE WAKAMATWE-DC
WAZAZI WASIOPELEKA WATOTO SHULE WAKAMATWE-DC
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment