Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wananchi wa Kata ya Isakamaliwa katika kijiji cha Isakamaliwa
wilayani Igunga wameikataa serikali ya kijiji mbele ya Mkuu wa wilaya
Elibariki Kingu.
Viongozi waliokataliwa ni Mtendaji wa kijiji Bw. Erasto Nshokoro,
mwenyekiti wa Kijiji Silasi Mguma pamoja na wajumbe wake 17 wa Serikali ya
kijiji.
Wananchi hao wakizungumza kwa masikitiko kwenye Mkutano wa hadhara
mbele ya mkuu wa wilaya wamesema Mtendaji wa kijiji pamoja na mwenyekiti
wameshindwa kusoma mapato na matumizi kwa miaka minne huku wakiendelea
kukusanya fedha toka vyanzo vya vijiji na kuendelea kujinufaisha wao wenyewe.
Wamesema pamoja na wananchi kuomba mikutano ya kusomewa mapato na
matumizi, lakini mtendaji wa kijiji amekuwa akiwatishia hata kuwaweka ndani kwa
ajili ya kuficha maovu yake huku wakidai kwamba amekuwa akishirikiana
na wafugaji toka mkoa wa shinyanga akichukua fedha toka kwa wafugaji hao
na kusababisha migogoro baina ya wafugaji wa Isakamaliwa na Shinyanga hali
ambayo imekuwa ikileta uvunjifu wa amani katika kijiji chao.
Naye diwani wa kata ya Isakamaliwa Bw. Dotto Kwilasa amesema
pamoja na yeye kuagiza serikali ya kijiji kuwasomea mapato na matumizi
wananchi, lakini viongozi hao wameshindwa kutekeleza agizo lake na kusababisha
manung’uniko makubwa toka kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment