Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ZAIDI ya
wachimbaji wadogo wa dhahabu 7000 wilayani Nzega Mkoani Tabora wameiomba
serikali kupitia wizara ya madini kuwapatia Lesseni ya uchimbaji katika mgodi
mdogo wa dhahabu wa mwanshina uliopo pembezoni mwa mgodi mkubwa wa dhahabu wa
resolute.
Wakizungumza na
waadishi wa Habari katika mgodi huo wameiomba serikali iwapatie Lesseni ya
kuchimba dhahabu licha kuvamia eneo hilo kutokana na kukabiliwa na shida
mbalimbali za kimaisha.
Joseph Mabondo
Mwenyekiti wa wachimbaji hao alisema kuwa wachimbaji zaidi ya 7000 wamevamia
eneo hilo kwa ugumu wa maisha ikiwa na wengine kujiajiri na kuajiriwa ili
kuendesha maisha.
Amesema
kuwa watu hao 7000 walivamia eneo hilo na kuanza kufanya kazi za uchimbaji
madini huku umoja huo ukisimamia sheria ndogo ndogo za kulinda ulinzi na
usalama ikiwa na kutunza mazingira ya eneo husika.
Ameiomba serikali
kuptia wizara ya Nishart na Madini kuweza kutoa Lessen ya uchimbaji
wadogo ili wananchi waweze kujikwamua kiuchumi ikiwa na kuinua vipato v ya
maisha yao ya kila siku.
Mabondo ameitaka
serikali kutochukua majukum ya kufunga mgodi huo licha ya wananchi kujichukulia
hatua mikononi badara yake busara zitumike ikiwa na kuepusha mazara yanayo weza
kujitokeza kama vile uhalifu ikiwa na vurugu.
Mjumbe wa
shirikisho la wachimbaji wadogo kitengo cha dhahabu Nicodemas Majabe amesema kuwa
wachimbaji hao walisha wasilisha maombi yao ya kupatiwa Lesseni ya uchimbaji
kupitia wizara husika na shuguli za ufuatiliaji zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment