Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Wilaya (DC) ya Igunga, Elibariki Kingu, amemwagiza
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwafukuza kazi watumishi wawili wa
zahanati ya Kijiji cha Isakamaliwa kwa kudharau maelekezo yake ya
kuwataka warudi sehemu yao ya kazi.
Watumishi wa halmashauri wanaotakiwa kufukuzwa kwa kukaidi agizo la
mkuu wa wilaya ni Daktari wa zahanati, Fabian Malekela na muuguzi,
Joseph Raphael, ambao hivi karibuni walikutana na Kingu aliyewataka
warudi katika maeneo yao ya kazi.
Pia alimuagiza Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wilayani humo,
Manumbu Kalima, kuvunja mkataba na Anna Malongo kwa kushindwa
kutekeleza mkataba wa kuwahudumia wananachi.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment