Mkuu wa wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu, ameahidi kuwasomesha wanafunzi 4 waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Bukoko wilayani Igunga.
Kingu alitoa ahadi hiyo kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Bukoko Kijiji cha Ipumbulya wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara.
Amesema, ameamua kuwasaidia vijana hao kwa kuwa familia zao hazina uwezo wa kuwasomesha sekondari na kwamba akiwa Mkuu wa wilaya hayupo tayari kuona wanafunzi wakikatiza masomo yao kwa ukosefu wa Ada za shule.
Vijana watakaosaidiwa kusomeshwa ni Nkunda Seni, Maria Msengi, Msengi Israel na Mkoma Israel wote wakazi wa ka ta ya Bukoko.
Wakati huo huo Mkuu huyo wa Wilaya ametoa msaada wa Solar Power moja yenye thamani ya shilingi Milioni moja katika zahanati ya Bukoko na mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Ipumbulya.
Akitoa misaada hiyo, Kingu amesema amefurahishwa na wananchi wa Bukoko na Ipumbulya kwa kuitikia wito wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF ambapo katika mkutano huo baadhi ya wananchi walilipa shilingi 10 000/= kila mmoja na kujiunga rasmi na CHF na kukabidhiwa kadi tayari kwa matibabu.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment