Home » » MWANAMKE ACHOMWA KISU MGONGONI AKIDAIWA KUCHUKUA MUME WA MTU MKOANI TABORA

MWANAMKE ACHOMWA KISU MGONGONI AKIDAIWA KUCHUKUA MUME WA MTU MKOANI TABORA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Mariamu Hussein akiwa na hali mbaya baada ya kuchomwa kisu mgongoni na kwenye paja wakati alipovamiwa na mwanamke mmoja ambaye inadaiwa kuwa Mariamu alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wa mwanamke huyo.Katika mkasa huo ilielezwa kuwa Mariamu akiwa nyumbani kwao ghafla alifika mwanamke huyo na kudai kuwa amekuja
kutekeleza mauaji kwa kile kilichofahamika kuwa amekuwa akivumilia kwa muda mrefu kuchukuliwa mume wake pasipo kuleta fujo yeyote jambo ambalo lilionesha unyonge wa hali ya juu kwa mwanamke huyo ambaye alifika nyumbani hapo na kucharuka kama Mbogo aliyejeruhiwa na kuanza kufanya unyama huo.
 Mwanamke aliyefanya unyama huo,alilazimika kukimbizwa Kituo Kikubwa cha Polisi Tabora,.Mariam akiwa hoi taabani huku damu ikiendelea kububujika kwenye jeraha kubwa la mgongoni.  Mpini wa kisu alichochomwa Mariamu ambapo inasadikiwa Mwanamke huyo baada ya kumpiga kisu cha mgongoni na kuingia,kilikatikia mgongoni na kumfanya Mariamu azidiwe na kupoteza fahamu

PICHA NA JUMA KAPIPI

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa