Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
UHARIBIFU wa mazingira katika Mkoa wa Tabora imeelezwa ni mkubwa
kutokana na kukithiri kwa shughuli mbalimbali za kijamii zisizozingatia
kanuni za utunzaji wa mazingira.
Hayo yameelezwa na Meneja Miradi wa Taasisi ya Mwanza Sustainable
Environment Association (MSEA) Kanda ya Magharibi, Stan Fusi,
alipozungumza na waandishi wa habari mjini Tabora.
Alisema hali hiyo inatokana na wananchi wengi kutokuwa na elimu ya
utunzaji wa mazingira katika maeneo yao na kutoelewa matumizi bora na
uhifadhi wa maeneo yanayowazunguka.
Aidha, alisema taasisi yake kwa kushirikiana na serikali ya Mkoa wa
Tabora wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa uhifadhi
wa mazingira kwa kuwawezesha kushiriki zoezi la upandaji miti kupitia
mradi wa miombo.
Akifafanua zaidi alisema elimu hiyo imelenga kuwasaidia wananchi
kuzalisha mazao ya ‘timbau’ ambayo yanatokana na misitu zikiwemo mbao,
magogo na mazao mengine yasiyo ‘timbau’.
Meneja huyo alibainisha jitihada za kutoa elimu hiyo mpaka sasa
zimefikia kaya 12,500 kwa wilaya nne za Mkoa wa Tabora lengo likiwa
kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira.
Alizitaja wilaya hizo kuwa ni Urambo, Tabora Manispaa, Uyui na Sikonge.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment