Home » » WAJUMBE BUNGE LA KATIBA WATAKIWA KUJAWA NA HOFU YA MUNGU KATIKA KUTAFUTA KATIBA MPYA.‏

WAJUMBE BUNGE LA KATIBA WATAKIWA KUJAWA NA HOFU YA MUNGU KATIKA KUTAFUTA KATIBA MPYA.‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na Hastin Liumba,Tabora.
 

 
WAJUMBE wa Bunge maalumu la katiba mpya wametakiwa na kuaswa kuwa na
hofu ya Mungu pale wanapotenda kazi zao katika mijadala ya kutafuta
katiba mpya ndani ya Bunge maalumu la Katiba.
 
Kauli hiyo ilitolewa na Padri wa kanisa Katoliki jimbo la Tabora
mjini, Padri Leons Maziku wakati wa ibada ya hitimisho la kongamano
kwa vijana wa sekondari na vyuo lililofanyika katika kituo cha
wanafunzi  mkoani humo.
 
Padri Maziku alisema wapo baadhi ya wanasiasa,viongozi wa taasisi za
serikali na makundi mengine ya kijamii wamefikia hatua ya kuona nchi
kama mali yao na kutotambua kuwa nchi ni mali ya wananchi.
 
Alisema kama nchi tunatakiwa kuliombea bunge maalumu la katiba ili
wajumbe wake wawe wazingatifu wa matakwa na matarajio ya watanzania
yaliyoainishwa katika rasimu ya pili ya katiba na ytume ta mabadiliko
ya katiba.
 
Aidha aliongeza ifikie mahali wajumbe hao kuheshimu maoni ya
watanzania na muboresha maoni kwa hekima na busara ili kulinda
mustakabali wa taifa letu na Tanzania yenye amani kwa ustawi wa watu
wote.
 
Padre Maziku alisema tume ya mabadiliko ya katiba imewasilisha kwenye
bunge maalumu la katiba rasimu ya katiba mpya iliyotokana na maoni
huru ya watu binafsi,makundi mbalimbali zikiwemo taasisi za dini
,mamlaka za kiserikali na asasi huru za kiraia hivyo mawao hayo
yaheshimiwe.
 
‘Tunalisihi na kulishauri Bunge maalumu la katiba kuheshimu mawazo
yaliyowasilishwa na kutumia busara zilizopendekezwa na kujenga muundo
wa muungano utakaokidhi mahitaji ya
utangamano,mshikamano,amani,maadili,uhuru na uwajibikaji viongozi na
raia wa Tanzania.’ aliongeza.
 
Padri Maziku aliongeza siku zote wakati wa dhambi ya kifo husababisha
kujitenga,lakini uhuru,amani na furaha huleta kuungana ndivyo
iliyotokea kwa Adam na Eva,lakini siku zote wanatenda dhambi hukaa
mbali na mwenyezi Mungu.
 
Aidha alisisitiza zaidi kwamba watanzania bila shaka moja ya mihimili
mikubwa ya umoja ni uongozi bora na Mungu aliwatoa watu wake utumwani
Misri na kuwaweka huru kwa kuwateulia viongozi miongoni mwao hii
inapaswa kueleweka kwa viongozi wetu.
 
Hata hivyo alionya na kusema kuwa katika ulimwengu wa leo tunashuhudia
madhara ya utengano wa namna  dhambi nyingi za binadamu zinasababisha
mifarakano na vita na hayo ni matukio ya kila mara katika nchi nyingi
ulimwenguni na hasa kwetu Afrika.
 
“Iko mifano hai katika historia zetu wenyewe kila mara  matukio mengi
ya jamii kufarakana na kujiingiza kwenye vita.”aliongeza Padri Maziku.
 
Aidha alisema tulipopata uhuru tulichukua hatua kubwa kuunganisha nchi
mbili huru  za Tanganyika na Zanzibar na kuwa nchi moja ya Jamhuri  ya
Muungano wa Tanzania ikiwa ni kielelezo kwa bara la Afrika cha kujenga
umoja hivyo viongozi wetu wasifikie kuharibu hayo mazuri.
 
Ailiongeza na kuasa watazania na viongozi kwa ujumla kumshukuru Mungu
kwa nchi yetu kuwa kimbilio la waliokata tamaa lakini hivi sasa
zimejitokeza athari kadhaa zilizofanya umoja wetu upoteze baadhi ya
sifa zake za awali kwa sababu za ubinafsi wa watu,makundi na viongozi
wachache wasioitakia nchi mema.
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa