Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI ya Kijiji cha Mwanzugi, wilayani Igunga, Tabora imepiga
marufuku wananchi kutembea na nguo za ndani baada ya kuogelea katika
bwawa la kijiji.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, Mtendaji wa
Kijiji, Stanly Ngassa, alisena baadhi ya wananchi wamekuwa na tabia ya
kutembea na nguo za ndani mitaani baada ya kuongelea.
Alisema maamuzi hayo yataambatana na hatua kali za kinidhamu kwa wale
wote watakaobainika na kuvunja maadili ya Kitanzania na kukiuka
maamuzi ya kijiji.
Alisema serikali hiyo inapenda wananchi waogelee na kupumzika katika
siku za mapumziko na kuongeza kuwa maadili ya Mtanzania yalindwe kwa
hali na mali, ili kukilinda kizazi kijacho dhidi ya mabadiliko ya
maadili.
“Tutahakikisha wote watakaobainika kutenda kosa hilo watafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma hizo, kwani hatutakubali kuona kitu hiki
kinaendelea kutendeka na sisi tuliopewa dhamana tupo, lazima sheria
ichukue mkondo wake,” alisema Ngassa.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment