Home » » SERIKALI YA KIJIJI YAPIGA MARUFUKU KUONGELEA OVYO KWENYE BWAWA LA KIJIJI‏

SERIKALI YA KIJIJI YAPIGA MARUFUKU KUONGELEA OVYO KWENYE BWAWA LA KIJIJI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
SERIKALI ya Kijiji cha Mwanzugi wilayani Igunga Mkoani Tabora imepiga
marufuku wananchi kuogelea katika bwawa la kijiji bila kufuata maadili
ya kitanzania ikiwemo kutembea wakiwa na nguo za ndani.
 
Akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake Mtendaji wa kijiji
,Stanly Ngassa  alisena baadhi ya wananchi wamekuwa na tamaduni za
kuvunja maadili ya kitanzania kwa kutembea na nguo zao za ndani katika
vitongoji vya kijiji hicho bila kujali wakata na mazingira.
 
Alisema wananchi hao wamekuwa wakiogelea siku za mapumziko kama
kubadilishana mawazo baadhi yao hujikuta wakitoka na nguo hizo hadi
mitaani hali inayo sababisha kuvunja utamaduni wa mtanzania ikiwa na
kuwafundisha vibaya watoto wa maeneo hayo.
 
Mtendaji huyo alieleza serikali ya kijiji ilikutuna kwa haraka baada
ya kuona hali hiyo imejitokeza kwa nyakati mbalimbali katika siku za
mapumziko mwisho wa wiki na kufikia hatua ya kutoa kauli hiyo ya
kupiga marufuku kutembea na nguo za ndani wakiwa katika vitongoji.
 
Alisema kuwa maamuzi hayo yataambatana na hatua kali za kinidham kwa
wale wote watakao bainika na kuvunja maadili ya kitanzania na kukiuka
maamuzi ya kijiji.
 
Alisema kuwa serikali hiyo inapenda wananchi waongelee na kupumzika
katika siku za mapumziko ya wiki na kuongeza kuwa maadili ya mtanzania
yalindwe kwa hali na mali ili kukilinda kizazi kijacho dhidi ya
mabadiliko ya maadili.
 
‘’Tutahakikisha wote watakao bainika na suala hilo watafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma hizo zitakazo wakabili kwani hatuta kubali
kuona kitu hiki kina endelea kutendeka na sisi tulio pewa dhamana tupo
lazima sheria ishike mkondo wake’’ Alisema Mtendaji huyo wa kijiji
Stanily  Ngassa.
 
Alitoa wito kwa viongozi wa serikali wilayani hapo kuiunga mkono
serikali hiyo ya kijiji katika kupinga vitendo hivyo viovu ambayo
vinalenga kuuruga utamaduni wa mtanzania ikiwa na kuhalibu kizazi cha
sasa hususani kijijini hapo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa