Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kwa
muda wa siku tatu sasa walimu zaidi ya 100 wanaofundisha katika shule
za msingi na sekondari sehemu mbalimbali wilayani Igunga, mkoa wa
Tabora, wameweka kambi katika ofisi ya Mkurungezi wa halmashauri ya
wilaya hiyo, wakimshinikiza kulipwa mishahara yao ya Aprili na Mei mwaka
huu.
Licha ya kuweka kambi, lakini pia wamechukua uamuzi wa kumfungia ofisini Kaimu Mkurungezi wa halmashauri hiyo, Sisti Kessy kwa muda wa saa nne ili walipwe fedha zao.
Akizunzumza kwa niaba ya wenzake, John Ambele, alisema wamekuwa wakiishi kwa shida kutokana na kutokuwa na fedha za kujikimu kwa kipindi cha miezi miwili sasa.
Alisema licha ya kukosa fedha za kujikimu, pia kodi ya nyumba nayo imekuwa tatizo kubwa, huku wenye nyumba wakidai kodi ya pango na baadhi ya walimu wamefukuzwa kwenye nyumba kutokana na kutolipa.
Alisema hawaondoki eneo hilo hadi wapate uhakika wa fedha zao, kwani walimu wengine walioajiriwa tayari wamelipwa kama kawaida.
Mwalimu huyo alisema wameamua kumfungia ofisini Mkurugenzi ili ujumbe uweze kufika katika mamlaka husika kwani wamechoka na ahadi za uongo zinazotumiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.
Hata hivyo, Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Igunga alifika eneo hilo na kuwaomba walimu hao wamfungulie mlango wa ofisi ya Mkurugenzi ili aweze kuzungumza nao na kukubali ombi hilo.
Akizungumza na walimu hao, Mkurugenzi aliwajulisha kuwa fedha hakuna hivyo wanatakiwa wavumilie hadi Juni 30, mwaka huu, jambo ambalo lilipingwa na walimu hao na huku wakigonga meza na wengine wakibubujikwa na machozi ambapo Mkurugenzi na wenzake walirudi Ofisini kufanya kikao.
Waliporudi kwa mara ya pili, Kaimu Mkurugenzi alisema halmashauri itawakopesha walimu hao waweze kujikimu hadi hapo fedha zao zitakapofika.

“Ndugu zangu walimu, tumeona tuwakopeshe Sh. 100,000 kila mmoja
ambayo itawasaidia mpaka mwisho wa mwezi huu mtakapoijia mishahara yenu
yote ya miezi mitatu” alisema.
Tamko hilo lilipingwa vikali na walimu hao na kusema kuwa hawatapokea fedha za kukopeshwa, wanachotaka ni fedha zao zote. “Tutapiga kambi katika halmashauri hii mpaka atakapokuja Mkuu wa Wilaya ili aje atueleze ni kwa nini walituahidi pasipokuwapo matumaini ya kulipwa fedha.”
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi alisema kuwa walimu wapya 298 wa shule za sekondari na msingi wanadai mishara ya Aprili na Mei inayofikia jumla ya Sh. 150,000,000 ambazo wao kama halmashauri wanas

0 comments:
Post a Comment