Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umetenga sh bilioni 10
zitakazokopeshwa kwa watoa huduma, ili kuboresha huduma kwa wanachama
wake.
Kaimu Mkurugenzi wa NHIF, Hamis Mdee, alibainisha hayo mjini hapa
mwishoni mwa wiki katika taarifa yake kwenye mkutano wa wadau.
Mdee alisema mfuko huo umetenga fedha hizo, ili kuhakikisha wanachama wanapata huduma bora za vipimo.
Alisema fedha hizo zitakopeshwa kwa watoa huduma, ili kuwawezesha kupata vifaa tiba na kukarabati maeneo ya kutolea huduma.
Aidha, alibainisha utaratibu huo ni wa mikopo nafuu na marejesho yake
hayatafanyika kwa fedha taslimu bali kwa kutoa kwenye madai ya watoa
huduma yanayowasilishwa kwa ajili ya malipo.
Alisema bodi imeagiza menejimenti kuandaa utaratibu wa kuzizawadia
halmashauri zitakazofanya vizuri katika uandikishaji wanachama wa mfuko
wa CHF na nyanja nyingine.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment