Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri Christopher Chiza
Hayo yalisemwa na Waziri wa wizara hiyo, Christopher Chiza, baada ya kutembelea Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) na kutoa taarifa ya hali ya chakula na matarajio ya mavuno kwa mwaka 2014/15.
Alisema mpango huo umekuja baada ya serikali kufuta utaratibu wa kuwapa pembejeo wakulima kwa kutumia vocha.
Alisema katika msimu uliopita NFRA ilikuwa na asilimia 118 na hadi hivi sasa serikali ina jumla ya tani 176,062 ya chakula katika maghala yaliyopo Rukwa, Iringa, Mbeya na Songea.
“Usalama wa chakula ni usalama wa nchi msimu huu 2014/15 tutanunua tani 200,000 ikiwa ni mpunga na mahindi, NFRA kazi yake ni kuhifadhi chakula na si biashara, lakini mwaka huu tutauza akiba yake ya tani 75,000 katika soko la ndani na nje ya nchi ili kutoa nafasi, kupata mapato na kufanya ununuzi wa mazao,” alisema Chiza.
Alisema Juni 5, mwaka huu NFRA ilikuwa imekwishauza tani 24,490.6 kwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), taasisi na asasi nchini tani 5,000 na kwamba tani 50,000 zitauzwa katika nchi jirani ili kukuza soko.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment