Na Mwandishi Wetu, Tabora
Watu
   16 wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 750 kujeruhiwa  baada
 ya mabasi waliokuwa wakisafiria kugongana katka k ijiji  cha Mlogolo 
wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Ajali
 hiyo imetokea leo hii jioni majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la 
Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea 
Mbeya kwenda  Mwanza kumegongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline 
lenye namba za usajiri  T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kupitia 
Mpanda.
Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani   Sikonge.
Pia
 inadaiwa kuwa madereva wa mabasi hayo wamefariki huku yule wa basi la 
Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe akiwa amekatika kiwiliwili 
na  kuwa jitihada za kutafuta kichwa  chake zilikuwa zikifanyika baada 
ya kupondeka vibaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi( Day-worker)
na mwendo kasi na imeelezwa kuwa  karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.
Mabasi
 yaliyohusisha ajali hiyo ni basi la  Sabena lililokuokea  Mbeya kwenda 
-Mwanza na AM Dreamline lililokuokea  Mwanza kwenda Mpanda.
 Kamanda
 wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP). Suzana 
Kaganda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja walikufa kuwa 
ni 17 pamoja na majeruhi hao 75 na kuwa Polisi wanafanya uchunguzi 
kuhusiana na ajali hiyo.




Baadhi ya miili ya marehemu.
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
1 comments:
SO SORRY FOR THEM
Post a Comment