Na Mwandishi Wetu, Tabora
Watu
16 wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 750 kujeruhiwa baada
ya mabasi waliokuwa wakisafiria kugongana katka k ijiji cha Mlogolo
wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Ajali
hiyo imetokea leo hii jioni majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la
Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea
Mbeya kwenda Mwanza kumegongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline
lenye namba za usajiri T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kupitia
Mpanda.
Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani Sikonge.
Pia
inadaiwa kuwa madereva wa mabasi hayo wamefariki huku yule wa basi la
Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe akiwa amekatika kiwiliwili
na kuwa jitihada za kutafuta kichwa chake zilikuwa zikifanyika baada
ya kupondeka vibaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi( Day-worker)
na mwendo kasi na imeelezwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.
Mabasi
yaliyohusisha ajali hiyo ni basi la Sabena lililokuokea Mbeya kwenda
-Mwanza na AM Dreamline lililokuokea Mwanza kwenda Mpanda.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP). Suzana
Kaganda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja walikufa kuwa
ni 17 pamoja na majeruhi hao 75 na kuwa Polisi wanafanya uchunguzi
kuhusiana na ajali hiyo.
Baadhi ya miili ya marehemu.
1 comments:
SO SORRY FOR THEM
Post a Comment