Home » » NZEGA YAPUNGUZA VIFO VYA MAMA, MTOTO

NZEGA YAPUNGUZA VIFO VYA MAMA, MTOTO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WILAYA ya Nzega, mkoani Tabora imefanikiwa kupunguza vifo vya mama na mtoto  kutokana na  wanaume kududhuria kliniki za wenzi wao pamoja na kufuata taratibu na masharti  ya afya  ya mama na mtoto.
Akizungumza katika makabidhiano ya vifaatiba vya mama na mtoto vilivyokabidhiwa na shirika lisilo la kiserikali Tabasamu, Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto Wilaya, Taus Kibonge, alisema takwimu zinaonyesha mwaka 2012 wilaya ya Nzega ilikuwa na vifo vya mama na mtoto 131 kati ya watu 100,000, lakini mwaka 2013 imepungua hadi kufikia vito 123 kati ya watu 100,000 kutokana na uwajibikaji utoaji wa elimu dhdi ya wananchi.
Alisema malengo ya serikali ni kupunguza vifo hivyo kwa kiwango kikubwa kwa ushirikiano na mashirika mbalimbali ya kiserikali na yale yasiyo ya kiserikali.
Alisema vifaa vya mama na mtoto vilivyokabidhiwa hospitali hapo vitachangia kupunguza maradufu tatizo hilo na kuwataka wananchi kuongeza jitihada za kukabiliana na tatizo hilo.
Akikabidhi vifaa hivyo, Mratibu wa Care International kupitia mradi wake Tabasamu, Philipina Kihupi, alisema shirika hilo limetoa vifaatiba vyenye thamani ya zaidi sh. milioni 160 vitakavyowasaidia mama na mtoto.
Alisema vifaa hivyo vitanufaisha vijiji 36, kata 30 zote zikiwa za wilaya ya Nzega na kuongeza kuwa watumishi wa afya wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu ikiwa na kutunza vifaa hivyo.
Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa wilaya ya Nzega, Bituni Msangi, alisema wanaume wanapaswa kusimama kidete kuhakikisha wanaambatana na wenza wao kuhakikisha wanapata huduma ya afya na mtoto.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa