Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SHIRIKA la Posta mkoani Tabora, wametembelea kituo cha watu wasiojiweza cha Kanisa Katoliki kilichoko katika manispaa ya Tabora na kutoa misaada ya mbalimbali.
Misaada waliyotoa ni Juisi katoni tatu, sukari kilo 25, sabuni katoni tatu, mafuta ya kula lita 10 na biskuti boksi moja vyote vikiwa na thamani ya sh 200,000.
Akizungumza na waandishi wakati wa ziara hiyo Kaimu Meneja wa shirika hilo mkoani Tabora, Mwantunu Tambwe, alisema wameamua kutoa misaada hiyo katika kuadhimisha Siku ya Posta duniani.
Alisema kutokana na kile wanachopata katika kazi zao za kila siku kama shirika, wakaona ni sahihi kutembelea kituoni hapo na kutoa misaada hiyo.
Aidha, Kaimu Meneja huyo alitoa wito kwa jamii na mashirika mengine kutembelea na kutoa misaada kulinhana na mahitaji ya watu waishio kwenye mazingira hayo.
“Msaada huu ni kidogo, lakini kutokana na kile tunachopata kama shirika tumeona tukigawe kwa hawa wenzetu tunaomba wengine wasisubiri kuona wengine wamefanya hivi wajitoe tu kusaidia,”alisema.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment