Mkoani Tabora, shule nne zimefungwa kutokana na wazabuni kusitisha huduma kutokana na kuidai Serikali zaidi ya Sh bilioni 1.5 za chakula walichokisambaza kwa shule mbalimbali.
Mapema mwezi Februari mwaka huu, ofisi ya
katibu tawala mkoa wa Tabora iliandika barua kwenda Tamisemi ikielezea ukubwa wa madeni ya wazabuni na yasipolipwa watasitisha huduma kama
ilivyotokea hadi shule zimefungwa.
Sekondari zilizofungwa ni Kazima ambayo wanafunzi wote wamerudishwa makwao isipokuwa wale wa kidato cha sita ambao wamepewa maelekezo ya kuwa wavumilivu kwani watabaki wakijiandaa kwa ajili ya kufanya mitihani.
Baadhi ya wanafunzi waliorudishwa makwao kutoka Shule ya Sekondari Kazima, wamesema walipewa taarifa kwa mdomo na walimu wao, kwamba
watatakiwa kurudi shuleni hapo Aprili 24 ama watakapotangaziwa vinginevyo.
Shule nyingine iliyofungwa ni Sekondari ya Wavulana Tabora ambapo kwa mujibu wa mwalimu ambaye hakutaka kutaja jina lake, wanafunzi wote wamerudishwa majumbani kwao na kubakishwa wa kidato cha sita tu wanaojiandaa kwa mitihani yao ya mwisho.
Kwa mujibu wa mwalimu huyo, shule hiyo kongwe mkoani Tabora na nchini kwa ujumla yenye zaidi ya wanafunzi 700, imebakisha 131 wa kidato cha sita pekee.
Sekondari nyingine ambazo pia zimefungwa kutokana na kadhia hiyo mkoani humo ni pamoja na Milambo na Tabora wasichana ambazo idadi ya wanafunzi waliorudishwa makwao haijafahamika.
CHANZO GAZETI LA MTANZANIA
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment