Na Godfriend Mbuya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli
wakati wa ziara yake mkoani Tabora alitoa maagizo kadhaa kwa watendaji likiwemo
agizo la kufunguliwa kwa stendi ya mabasi Igunga ambayo ilikamilika na kuacha
kutumiwa kwa miaka 10.
Kufuatia agizo hilo tayari SUMATRA kwa kushirikiana na jeshi
la polisi kikosi cha usalama barabarani wameanza kuelekeza magari yote ya
abiria uyanayopita Tabora eneo la stendi hiyo kuhakikisha yanapita jambo ambalo
limeanza kufanyiwa kazi kwa vitendo.
Akizungumza wakati wa kukagua utekelezaji wa agizo hilo Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri amesema SUMATRA washirikiane na jeshi
la polisi kuhakikisha kila gari la abiria linapita na dereva atakayekaidi agizo
hilo anyang'anywe leseni.
Ni lazima mabasi yapite hapa stendi na yeyote
atakayekaidi SUMATRA chukueni hatua na jeshi la polisi toenio ushirikiano
kuhakikisha suala hili linafanikiwa'' Amesema Mwanri.
Aidha kwa upande wao wananchi wamesema watanufaika sana
kufuatia stendi hiyo kuanza kufanya kazi kwa kuwa watafanya biashara mbalimbali
kuzunguka stendi hiyo.
You might also like:
0 comments:
Post a Comment