Afisa
Tawala Wilaya ya Tabora mjini Mhe.
Sweetbert Nkuba, (kushoto)
akipokea moja ya madawati 90 yaliyotolewa na Dr.Amon Mkoga Foundation na
kukabidhiwa kwake na mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndugu.Amon Mkoga(kulia).
Anayeshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka
ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah
Kibonde Msika ambao ni wadhamini wa kampeni hiyo iitwayo “Simama Kaa”
Ndugu.Amon Mkoga akiwa pamoja na wanafunzi hao baada ya kukabidhi madawati hayo
Ndugu.Amon Mkoga akiwa amekaa na baadhi ya wanafunzi baada ya kukabidhi madawati hayo
Taasisi
ya Dr.Amon Mkoga Foundation imetoa msaada wa madawati 90 yenye thamani
ya shilingi milioni 5.5 kwa shule za msingi katika manispaa ya Tabora,
ikiwa ni mchango wa Taasisi hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini.
Akizungumza
leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa
wilaya Tabora mjini , Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndugu Amon Mkoga
amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya taasisi hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.
“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Dr.Amon Mkoga Foundation katika
kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini
kwamba kupitia msaada huu, Taasisi yetu inatoa mchango wake katika
kujenga viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali
wakiwamo madaktari, wahandisi na wengineo, “amesema Mkoga.
Makabidhiano yalihudhuriwa na Afisa Tawala Wilaya ya Tabora mjini Mhe. Sweetbert Nkuba
ambaye alisema madawati hayo 90 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa
watoto katika Mkoa wa Tabora na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga
mkono zoezi hilo.
0 comments:
Post a Comment