KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mfuko wake maalumu wa
kusaidia jamii wa Airtel FURSA Tunakuwezesha, imekabidhi hundi ya Sh
milioni 20 kwa Mbunge wa Nzega Mjini, Hussen Bashe, kuwanufaisha
wajasiriamali jimboni humo.
Akikabidhi hundi hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colasa
alisema, “Airtel imejipanga kuhakikisha vijana wanaendelea kunufaika na
mradi wa Airtel FURSA kwa kuwapatia misaada ya kukamilisha mipango yao
waliyoipanga ya kupunguza changamoto walizonazo ikiwamo ya ukosefu wa
ajira na mtaji ili watimize malengo yao kibiashara”.
Bashe aliishukuru Airtel na kuahidi kusimamia mradi huo wa ukopeshaji
kwa ajili ya kuweza kuinua vipato vya wananchi wa Nzega kama
ilivyokusudiwa.
Mradi wa Airtel Fursa, ulianzishwa Mei mwaka jana na tayari
umewafikia vijana zaidi ya 5,000 kutoka katika mikoa 10 nchini pamoja na
vijana 100 waliowezeshwa kwa kupewa mitaji na vitendea kazi.
Programu hii kati ya Airtel na Mfuko wa Maendeleo Nzega chini ya
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini, Bashe, itawawezesha zaidi ya
wajasiriamali 350 kunufaika na mikopo kupitia huduma ya Airtel Money.
CHANZO :HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment