Home » » MKUU WA WILAYA AWASWEKA NDANI VIONGOZI WATATU

MKUU WA WILAYA AWASWEKA NDANI VIONGOZI WATATU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkuu wa wilaya ya Igunga, Mkoani Tabora, John Mwaipopo ameagiza afisa mtendaji wa Kata ya Igunga Robert Mwagala pamoja na maafisa afya wa Kata hiyo, Ephraim Ezekieli na Restuta Malunguja kukamatwa na kuwekwa maabusu kwa kushindwa kusimamia suala la usafi.

Akizungumzia tukio hilo, Mwaipopo alisema kukamatwa kwa watumishi hao pia kulihusisha pia wakazi watano wakazi wa Mtaa wa Mwayunge waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma za kuchoma moto hovyo kwenye makazi ya watu.

"Haiwezekani serikali iwe inawalipa mishahara halafu maafisa watendaji wanashindwa kutekeleza majukumu waliyopewa... kamwe hali hiyo haitaweza kuvumiliwa," alisema Mwaipopo.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya alisisitiza kuwa watumishi hao waliokamatwa wataendelea kukaa mahabusu hadi hapo mbio za mwenge wa Uhuru zitakapomalizika ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Chanzo Nipashe

 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa