Home » » WAFANYAKAZI WA HOSPITALI WAKAMATWA NA DAWA

WAFANYAKAZI WA HOSPITALI WAKAMATWA NA DAWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


KATIBU Tawala Mkoa wa Tabora, Dk. Thea Ntara
Na Tiganya Vincent, Maelezo-TABORA
KATIBU Tawala Mkoa wa Tabora, Dk. Thea Ntara amemtaka Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Kitete kuwakamata na kuwafikisha polisi watumishi wawili wa hospitali hiyo wanaotuhumiwa kukutwa na dawa na vifaa tiba katika mikoba yao.
Kauli hyo aliitoa jana baada ya watumishi hao kukamatwa na vifaa hivyo ambavyo ni dawa na vifaa vya hospitali wakitaka kwenda kuviuza katika hospitali binafsi.


Alisema dawa na vifaa tiba hivyo havitakiwi kutoka nje ya hospitali na havikuwa na maelekezo ya mganga.
Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliwapongeza walinzi waliofanya kazi hiyo na kuwaagiza kuongeza kupekua watu wote wanaokwenda kuona wagonjwa kwa sababu inawezekana watumishi wengine ambao siyo waadilifu wakatumia fursa hiyo kutorosha dawa na vifaa tiba vingine.
Vifaa na dawa vilivyokamatwa ni Cannula, Surgical gloves, Syringesa, Urinal bag, IV giving set, Blood giving set, Brainded silk number, water injection, powder, soap, examination glove, gentamyacin injection ampule, ascorbic acid.
Hospitali hiyo imekuwa ikikumbana na wizi wa mara kwa mara hatua iliyosababisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuisimamisha kampuni iliyokuwa imepewa jukumu la kulinda.
Ofisi hiyo iliweka kampuni nyingine wakati taratibu za kuichukulia hatua kampuni ya awali zikiendelea.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa