POLISI mkoani Tabora inaendelea kuchunguza tukio la muuguzi wa Kituo
cha Afya Kata ya Igurubi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Damiana Mgaya
(26), kwa tuhuma ya kumbaka binti wa miaka 18 anayeishi Kitongoji cha
Mwagala B Kijiji cha Mwagala.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa alisema
wameanza uchunguzi wa uhalifu uliofanywa Julai 13, mwaka huu saa 8 hadi
alfajiri wakati binti huyo akimuuguza mama yake, Tatu Simbi aliyelazwa
kituo hicho cha afya baada ya kushambuliwa kwa kipigo na mumewe.
Mutafungwa alisema Mgaya alimpokea mama wa binti huyo akiwa hoi na
ndipo alimpatia matibabu, kisha kumlaza katika kituo hicho cha afya huku
akimchoma sindano ya usingizi, ambayo ilisababisha mama huyo kupitiwa
na usingizi.
Alisema muuguzi huyo alichoma binti huyo sindano ya usingizi, ndipo
alimwingilia kimwili na kumsababishia maumivu makali mwili mzima.
Alisema baada ya kuambiwa hivyo, binti huyo alikubali kuchomwa sindano
mbili na alipochomwa sindano ya kwanza aliishiwa nguvu na alipochomwa
sindano ya pili, alianguka na kupitiwa na usingizi hadi asubuhi.
Alisema baada ya kuona amelala pasipokuwa na fahamu, muuguzi huyo
alianza kumbaka hadi alfajiri alipoamshwa na mama yake huku yeye akiwa
hajitambui kutokana na maumivu aliyokuwa akiyasikia sehemu zake za siri
na mwili wote. Alisema kwa sasa binti huyo hali yake ya afya inaendelea
vizuri.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment