Na Tiganya Vincent
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri amewaonya wakazi mkoani hapa kuacha tabia ya uuzaji ovyo wa ardhi huku wao wakibakiza
eneo dogo la ardhi wanalolimiki ambalo haliwezi kutosheleza matumizi ya familia zao katika siku za baadaye.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Mwanri kwenye sherehe za kilele cha maonesho ya nane nane kwa
kanda ya Magharibi yalifanyika katika Viwanja vya Fatuma Mwasa mjini hapa.
Alisema kutokana na Mkoa
wa Tabora kuanza kufunga kwa kasi kwa kuwa na miundo mbinu mbalimbali
kama vile usafiri wa uhakika wa anga , kuanza ujenzi wa mradi mkubwa wa
maji kutoka ziwa Victoria, ujenzi wa reli ya kisasa na barabara za lami
zinaongeza fursa ya watu mbalimbali kuja mkoani
hapa kwa shughuli mbali.
Bw. Mwanri alisema watu hao wanaweza wakajitokeza na kuanza kuwarubuni wakazi ili wawauzie ardhi zao hata kwa bei ambayo
halingani na eneo husika huko wenyewe wakipata fedha kidogo ambazo hazimsaidii kujiendeleza bali kuendelea kuwa maskini.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa thamani ya ardhi inaongezeka kila siku na watu wanaohitaji wanaongezeka na hivyo ni vema
wakawa makini kabla ya kufanya maaumuzi ya kuuza vipande vyao vya ardhi ili wasije
wakajuta mara fedha walizolipwa zitakapokuwa zimekwisha.
Aliongeza kuwa hata kama mtu anataka kuuza eneo lake ni vema akajihakikishia kuwa lilobaki litaiwezesha familia yake kuwa
na mahali bora pa kuishi na kufanyia shughuli nyingine za uchumi kama vile kilimo na ufugaji wa kisasa.
Bw. Mwanri alisisitiza kuwa uuzaji wa ovyo wa ardhi ndio wakati mwingine umepelekea migogoro pindi wauuzaji wanapokuwa
wamemaliza fedha walizolipwa huku wao hawajafanya kitu na kuunza kuvamia maeneo ya wengine.
Mmoja
wa Wakazi wa Tabora Bi. Rebecca Alfred anapongeza hatua ya Mkuu wa Mkoa
kutoa angalizo hilo kwa wakazi wa Mkoa huo
na kusema kuwa migogoro mingi katika familia imesababishwa na baadhi ya
ndugu kuuza maeneo yao na wanapomaliza eneo yao wanaanza kuvamia ya
maeneo ya wenzao.
Alisema kuwa njia pekee ya kuondoa matatizo hayo ni pamoja na kupima maeneo yote ya wananchi na kuwapa hati ambazo wanaweza
kunufaika na huduma za mikopo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Bi
Rebecca alitoa wito Watendaji wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na
Biashara za Wanyonge nchini(MKURABITA) kuhakikisha
wanaharakisha kupima mashamba ya wananchi na kutoa elimu juu matumizi
bora ya ardhi ili kuwasaidia waweze kutumia ardhi yao kupata mikopo
badala ya kuuza kama sehemu ya kutafuta fedha na kila mtu kujua mipaka
yake.
Alisisitiza amesikia maeneo ambayo MKURABATA wamepima mashamba ya wananchi kumekuwepo na maendeleo hata kwa wananchi na
wamejua thamani ya ardhi na hakuna uuzaji ovyo ovyo.
0 comments:
Post a Comment