Na Tiganya Vincent

Alisema lengo la kuwapeleka vijana hao ni kutaka watakapotoka katika mafunzo hayo waweze kwenda kufundisha vijana wenzao juu ya fursa ya ufugaji nyuki kisasa unavyoweza kuwaondoa katika umaskini na kujipatia kipato kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alisema kuwa vijana wengi wakielimika juu ya ufugaji wa kisasa itasaidia upunguzaji wa uharibifu wa mazingira ikiwemo uchomaji moto unaosababishwa na watu wanakuwa wakivuna asali na ukataji wa magome kwa ajili kutengeneza mizinga ya asili.
Mmoja wa Vijana wanajihusisha na Ufugaji wa Nyuki Bw. Hussein Kapandamiti amepongeza hatua ya Mkuu wa Mkoa kutoa kuagiza vijana wapate mafunzo ya ufugaji nyuki ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha ili wapate fursa za kujiajiri wenyewe na wakati mwingine waajiri wenzao.
Alitoa wito kwa watakaopata fursa hiyo kuzingatia mafunzo watakayoyapata na kuja kuwa walimu kwa wenzao ili gharama itakayotumika iwe na tija kwa watu wengi.
Aidha Kapandamiti alitoa wito Taasisi zinazojihusisha na utengenezaji wa mizinga ya kisasa kupunguza gharama ili watu waachane na mizinga ya asili ambayo hutoa mavuno kidogo ya asali.
0 comments:
Post a Comment