Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Tiganya Vincent
RS-TABORA
21 AGOSTI 2017
Wakala
wa Huduma za Mistu Tanzanaia (TFS) imepanga kupanga miti katika hekta
182,000 kwa mwaka ili kukabiliana na uharibifu wa mistu ulitokana na
shughuli mbalimbali za binadamu katika mistu ya hapa nchini.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Afisa Mistu na Mtalaalamu , Mshauri wa Usimamizi
na Uhifadhi wa Mistu wa TFS Dkt. Ismail Aloo wakati akiongea kwenye
kikao cha utekelezaji wa randama ya ushirikiano wa usimamizi wa
rasilimali za mistu kanda ya magharibi.
Alisema
kuwa hali ya uharibifu wa mistu hapa nchini inatisha ambapo hekta
372,000 kila mwaka zinaharibiwa kutokana na kilimo cha kuhama hama ,
uchomaji mkaa, mifugo isiyozingatia ufugaji bora na uchanaji mbao
usiozingatia taratibu na sheria.
Dkt. Aloo aliongeza kuwa ili
kukabiliana na tatizo hilo juhudi zaidi zinahitajika katika upandaji
miti kwa ajili ya kuziba pengo la uharibifu wa mistu ambao umeifanya Tanzania kuwa uhaba miti kwa ujazo wa mita wa miti milioni 19.
Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa TFS Mtendaji Mkuu wa (TFS), Prof. Dos Santos Silayo
alisema kuwa ni marufuku kwa viongozi wa vijiji kuwaagiza wananchi
kufekya mistu katika maeneo wanayomiki kwa kisingizio cha uendelezaji wa
sehemu zao.
“Watendaji
wa Vijiji katika baadhi ya maeneo wanawalazimisha watu wanaomiliki
maeneo ambayo yana miti kuifyeka kwa kisingizio cha kuendeleza eneo
lao…hii sio sahihi”alisema Profesa Silayo.
Alisema
kuwa viongozi hao lazima watambue kuwa mistu ya hapa nchini ina thamani
ni lazima wahakikishe wanaitunza kwa kusimamia sera na sheria na sio
wao kuwa chanzo cha uharibifu.
Akifungua
kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwaagiza Wakuu wa
Wilaya mkoani Tabora kushirikiana na Watendaji wa TFS katika kuhakikisha
wanasimamia Sera na Sheria katika kuwaondoa watu wote waliovamia mistu
ya hifadhi.
Alisema
kuwa suala la kusimamia mistu na kuifanya iwe endelevu haliwezi kuwa
TFS pekee bali linahitaji nguvu za pamoja ikiwemo kutoka katika
Halmashauri husika.
Bw.
Mwanri alisema kuwa uharibifu ukiendelea katika mistu haitalaumiwa TFS
pekee bali hata viongozi wengine katika maeneo husika watabeba lawama
hizo.
“Kama tutashirikiana fahamu
kuwa hakuna jambo ambalo litatushinda katika kukabiliana na watu
wanaoharibu mistu na kutishia maisha ya wananchi” alisisitiza Mkuu huyo
wa Mkoa.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa aliwaagiza Watendaji mbalimbali kuanza kuelimisha
wananchi umuhimu wa matumizi ya majiko sanifu yanayotumia mkaa kidogo
ili kupunguza mahitaji ya nishati hiyo ambayo nayo ni miongoni mwa
matishio ya mistu.
0 comments:
Post a Comment