Na Tiganya Vincent
Tabora
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Kassim ametoa wito kwa Wakulima wa tumbaku
mkoani Tabora kuanza kujipanga ili waanze kilimo cha zao hilo kwa
kunununua mbolea kwa kutumia fedha zao badala ya kuendelea kutegemea
mbolea za mkopo kupitia vyama vya msingi.
Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana katika maeneo mbalimbali wilayani Uyui wakati akiwahutubia wananchi.
Alisema
kuwa hatua hiyo itawasaidia wakulima hilo kuwa na huru hata wakati wa
kupanga bei ya zao wanapokwenda kuwauzia wanunuzi wa tumbaku.
Waziri
Mkuu aliongeza kuwa tabia ya kuendelea kusubiri mbolea ya mkopo
inawafanya wakulima wengi washindwe kusonga mbele kwa sababu pesa nyingi
inakwenda katika kulipia deni la mbolea.
“Ndugu zangu wakulima watumbaku
ni vema kuanzia sasa mkaanza kujipanga kwa msimu ujao wa kilimo kwa
kununua mbolea kidogo kidogo ili ikiwezekana ulime kwa kutumia mbolea
ulionunua mwenyewe……..hali hii itakufanya uwe uhuru hata wa kuamua bei
unayotaka” alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Alisema
kuwa ni wakulima wakaanza kwa kununua kidogo dogo mbolea ya tumbaku
kupitia mapato yanayotokana na mauzo ya tumbaku yao kama hatua ya
kuelekea katika kujikomboa na kuondokana na utegemezi wa mbolea za
mikopo ambayo zimewaingiza katika matatizo mbalimbali ikiwemo kuwa siku
nyuma kimaendeleo.
Aidha
Waziri Mkuu amepiga marufuku Kampuni zinazonunua tumbaku hapa nchini
kununua zao hilo kutoka kwa Mkulima kwa njia ya fedha ya Kimarekani
(Dola) na kusema kuwa vitendo hivyo ndio vinasababisha unyonyaji
wakulima.
Alisema tumbaku yote kuanzia sasa itakuwa ikinunuliwa kwa fedha ya kitanzania na sio vinginevyo.
Mhe.
Majaliwa alisisitiza kuwa wakulima wengi hajui dola jambo ambalo
limefanya viongozi wengi wakiwemo wa vyama vya msingi kumibia mkulima.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu alisema kuwa mtu akayekamatwa ananunua
tumbaku ya mkulima kwa njia ya vishada Serikali haitamuachia na kama
atakuwa ana chombo cha usafiri kitashikiliwa na Polisi ili iwe fundisho
kwa watu wenye tabia ya kuwavizia wakulima walime kisha wao waende
kurubuni na kununua tumbaku yao kwa nia ya ulanguzi.
Alisisitiza
kuwa tumbaku yote itauzwa kupitia Vyama vya Msingi na sio vinginevyo na
mtu yoyote atakayekutwa akiuza tumbaku nje ya utaratibu wa Serikali
atachukuliwa hatua kali.
0 comments:
Post a Comment