Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
amewaagiza watumishi wote wa umma kuondoka maofisa na kwenda vijijini
kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ambazo yanasababisha
wasiendelee.
Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana wakati akiongea na watumishi wa Wilaya ya Uyi mkoani Tabora.
Alisema kuwa wakisha kuwasiliza wananchi warudi Ofisi kwa ajili ya
kujipanga namna ya kutatua kero na matatizo ya wananchi ambayo
yanakwamisha juhudi zao ya kujiletea maendeleo.
Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Tano ipo kwa ajili ya
kuwatumikia wananchi wote na hivyo imetoa dhamana kwa watumishi wa umma
wafanye kazi karibuni kwa kwenda vijijini ili kuwatumikia Watanzania
wote.
Aidha alionya kuwa Serikali hii haitawavumilia watumishi wa umma wenye
tabia za urasimu katika kuwatumikia na kutatua kero mbalimbali za
watanzania.
"Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote wa umma ambayo mwananchi
anakwenda kwake kwa mara ya kwanza kueleza shida yake kisha anamwambia
mwananchi arudi kesho na anaporudi kesho , anambia tena arudi kesho
.....mwisho mwananchi anaanza kukata tamaa ya kusaidiwa tatizo lake"
alisisitiza Waziri Mkuu.
Alisema kuwa mwanachi anapofika katika Ofisi za Umma kwa ajili ya
kutatuliwa tatizo lake asaidiwe haraka bila kuzungushwa zungushwa ili
aone Serikali yake ipo kwa ajili ya kumsaidia.
0 comments:
Post a Comment