Na Tiganya Vincent
12 Agosti 2017
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza
kukamatwa kwa wazazi wenye tamaa ya fedha ambao wamekuwa wakiwakatisha
masomo mabinti zao kwa ajili ya kuwaozesha.
Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana Wilayani Uyui katika mkutano wa hadhara
Alisema
kuwa kuanzia sasa Watendaji wanatakiwa kuwakata na kuwafikisha katika
vyombo vya dola bila woga wazazi wa binti na wale wa kijana wanakatisha
masomo ya watoto wa kike kwa lengo la kuwaozesha.
Waziri
Mkuu alisema kuwa Serikali haitawavulia wazazi na watu wanaochangia
kurudisha maendeleo ya wasichana kisingizio cha kuwafungisha ndoa wakati
bado ni wanafunzi.
"Nawaagiza
Watendaji wote kuwakata wazazi wa binti na wale kijana ambao mtawakuta
wakiwa wanawaozesha mabinti wao ambao kimsingi walipaswa kuwa
shule......msimuogope mtu wakamateni wote wawe wazazi wa binti hata wa
yule anayetarajia kuoa ili hatua kali za kisheria dhidi yao ziweze
kuchukuliwa" alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Aliwaonya
pia vijana ambao wanamiliki na kuendesha pikipiki maarufu kama boda
boda ambao wamekuwa wakiwapakia wanafunzi kwa lengo la kuwarubuni ili
wajihusishe na vitendo vya ngono kuacha mara moja.
Waziri Mkuu alisema mtu atakayekamatwa Serikali itamfikisha Mahakamani ili aweze kupata adhabu kali.
Alisisitiza kuwa ni vema wakaacha wanafunzi hao wakasoma na sio kuwarubuni.
Mkoa wa Tabora ni miongoni mwa mikoa mitatu hapa nchini inayoongoza kwa mimba na ndoa za utotoni.
0 comments:
Post a Comment