Na Tiganya Vincent
Tabora
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaagiza
Wakuu wa Wilaya kusimamia zoezi la kuhakiki idadi ya wakulima wa
tumbaku na ukubwa mashamba ambayo wanaweza kulima kwa ajili ya kuweka
mipango mizuri ya uagizaji wa pembejeo kulingana na mahitaji halisi.
Mhe.
Majaliwa alitoa kauli hiyo jana mjini Tabora wakati wa kikao cha
majumuisho ya ziara ya siku nne mkoani hapo kuhimiza shughuli mbalimbali
za maendeleo na vile vile kufuatilia zao la tumbaku.
Alisema
kuwa lengo kutaka kuboresha uzalishaji wa zao hilo na kuweka mazingira
ambayo mkulima hataendelea kunyonywa na baadhi watu ambao hawalimi
tumbaku lakini ikifika wakati wa uuzaji wanajifanya nao ni wakulima wa
tumbaku.
Waziri
Mkuu aliongeza kuwa hatua hiyo pia itasaidia wataalamu wa eneo husika
kuweza kujua kwa haraka mahitaji ya wakulima wa zao la tumbaku katika
eneo lake na hivyo kuwasaidia ili waweze kuzalisha kwa wingi na tumbaku
iliyo katika kiwango bora
Aidha
Mhe. Majaliwa alisisitiza kuwa msimamo wa Serikali ni kuwa kila mkulima
atauza tumbaku yake kupitia Chama cha Msingi na atapaswa awe
amesajiliwa na Chama kilichopo katika eneo lake na sio vinginevyo.
Waziri
Mkuu alisema kinyume cha hapo mtu yoyote awe Mwanasiasa au mtumishi wa
umma atakayekamatwa anajihusisha na ununuzi wa tumbaku au uuzaji wa
pembejeo za kilimo kinyume na maelekezo ya Serikali atakamatwa na hatua kali dhidi yake zitachukuliwa.
Mhe. Majaliwa aliziaagiza Kamati
ya Ulinzi na Usalama kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Kijiji kukamata watu
wote bila kuwaonea huruma wale wananunua tumbaku kwa njia ya vishada na
wale wanaojihusisha na uuzaji wa mbolea kwa wakulima bila kuwa na
vibali.
0 comments:
Post a Comment