Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye shati jeupe ) akiongozana na viongozi mbalimbali kukagua mitambo ya Kiwanda cha Pamba cha Manonga jana wilayani Igunga kwa ajili ya kujionea hali halisi kilivyo hivi na mahitaji yake ili kianze upya uzalishaji.
Na Tiganya Vincent- RS-Tabora
SERIKALI
ya Mkoa wa Tabora imeawaagiza Maafisa Ugani kuanza mapema maandalizi ya
kilimo cha pamba kwa wakulima kutoka wilaya tano mkoani hapo
zilichaguliwa kulima zao ili waweze kuzalisha pamba nyingi na nzuri kwa
ajili viwanda mbalimbali hapa nchini.
Agizo
hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri jana wilayani
Igunga wakati alipokwenda kujionea hali halisi ya Kiwanda cha Pamba cha
Manonga wilayani Igunga ambacho kimekuwa hakifanyi kazi kwa miaka zaidi
ya 20 kwa sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa pamba ya kutosha.
Alisema
kuwa watendaji wote wanaohusika na usimamizi wa zao la pamba ni vema
wakahakikisha kuwa wakulima wanapanda mbegu zinazotakiwa na kwa nafasi
inayoshauri kitaalamu na kutimia mbolea na dawa za kuua wadudu
zinazotakiwa.
Mwanri
alisema kuwa Tabora imepata mbegu bora tani 500 ambazo zitasaidia
kusambazwa katika Wilaya ambazo zimechaguliwa kulima zao la Pamba za
Kaliua, Urambo, Nzega, Igunga na Uyui.
Alisisitiza pamba itakayolimwa na kuvuna itauzwa kupitia Vyama vya Ushirika na sio vinginevyo ili kuepuka mkulima kunyonywa.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa alipiga marufuku matumizi ya mbegu ambazo
hazikuidhinishwa na Bodi ya Pamba na kuingiza mkoani hapa dawa ambazo
zimepitwa na wakati.
0 comments:
Post a Comment