Na Tiganya Vincent
RS –TABORA
HADI hivi saa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora linawashikiria watu 44 wa kijiji cha
Mwamabondo wilayani Uyui kwa tuhuma za kuwashambulia silaha za jadi na
kuwauunguza kwa moto wanawake waanne wakiwatuhumu kuwa wachawi na
wanahusika na kifo cha mume wa mmoja wao.
Kauli
hiyo imetolewa jana mjini hapa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora
Wilboard Mtafungwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisini
kwake.
Alisema
kuwa idadi hiyo inafuatia 37 kukamatwa na kuunganishwa na wale saba
ambao walikamatwa hapo awali kufuatia tukio hilo na kufikisha 44.
Kamanda
Mtafungwa alisema kuwa wanawake hao walitendewa unyama huo na
wanakijiji hicho baada ya kuwakamata na kuwahoji kuhusiana na thuma za
kufanya vitendo vya kishirikina hapo kijijini.
Alisema
baada ya kuwahoji wanakijiji walipitisha azimio kuwa wakinama hao
wauwawe kwa kuchoma moto na ndipo walipofungwa vitambaa usoni wakiwa
uchi na kusambuliwa na fimbo sehemu mbalimbali za miili yao kisha
wakaanza kukusanya kuni na nyasi kwa lengo kuwachoma ili wateketee
kabisa.
Kamanda
Mtafungwa alisema kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema
wanaochukizwa na vitendo hivyo vya kikatili, waliamua kutumia askari wakiwa doria katika eneo la vijijini ili kuokoa maisha ya wanawake hao.
Alisema
kuwa chanzo cha tukio zima ni kifo cha Mafumba Tilawisi ambaye alikuwa
mume wa mmoja wa wanawake walioshambuliwa Manugu Lutema .
Kamanda
Mtafungwa alisema kuwa baada ya kifo chake taarifa zilisambaa na watu
wakakusanyika kwa ajili ya maandalizi ya mazishi na ndipo zilianza
kujitokeza tuhuma kuwa marehemu aliwawa kwa njia za kishirikina na mke
wake Manugu Lutema.
Alisema
kuwa ndipo watu wenye hasira waliamua kumukamata na kutaka ataje
wenzake anaoshirikiana nao katika vitendo vya kishirikina na ndipo
aliwataja wengine kwa hofu kuwawa ambao ni Elizebeth Kashindye, Maria
Sahani, Manugwa Lutema na Rahaeli Mikomangwa.
Kamanda
Mtafungwa alisema kuwa msako huo utaendelea hadi wale waliohusika na
tukio hilo wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya Sheria.
0 comments:
Post a Comment