Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Tiganya Vincent
WATU
saba wa kijiji cha Mwambondo wilayani Uyui wanashirikiliwa na Jeshi la
Polisi kwa tuhuma za kuwashambulia na kuwauunguza kwa moto wanawake
waanne wakiwatuhumu kuwa wachawi na wanahusika na kifo cha mume wa mmoja
wao.
Kauli
hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri
wakati wa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa alizozipata
kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa huo Wilbroad Mtafungwa.
Alisema
kuwa chanzo cha vitendo hivyo vya kinyama zilianzia baada ya Mtu mmoja
alikuwa akiitwa Mafumba Jirawisi kufariki kwa sababu ya maradhi lakini
baadhi ya watu walianza kumtuhumu mke wa marehemu anayeitwa Manugwa
Lutema kuhusika na kifo cha mume wake na kuamua kumpeleka porini na
kuanza kumshambulia huku wakitaka awaeleze watu wanaoshirikiana naye
kuwafanya vitendo vya kichawi.
Mwanri
alisema kuwa mama huyo baada ya kupiga sana na kuumia aliamua kutaja
ovyo majina ya majirani zake na ndipo nao wakaunganishwa naye na
kuendelea kupigwa na kuunguzwa katika sehemu za siri.
Kufuatia
vitendo hivyo vya kinyama Mkuu huyo wa Mkoa amemwagiza kuwasaka watu
waliobaki ambao wamehusika katika kitendo hicho wakiwemo Makamanda wa
sungusungu ili hatua kali ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Mmoja
wa majeruhi wa tukio hilo la kinyama alisema kuwa alilazimika kutaja
majirani zake ili kutaka kunusu roho yake baada ya kuona mashambulizi
yanazidi na anasikia maumivu makali.
Kwa
upande wa ndugu wa waathiri wameomba wagonjwa wao watibiwe bure kwa
sababu tukio hilo limetokea wakati wakiwa hawana kitu na hawajiandaa na
kutokuwa na fedha ya kulipia matibabu
Akijibu
ombi la ndugu hao Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunin Kamba
alisema wagonjwa wote walijeruhiwa na kuuguzwa moto watapewa matibabu
kwa mkopo katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa ya Kitete ,malipo
yatafanyika baadaye.
Alisema kuwa lengo ni kutaka kwanza kuokoa maisha yao kutokana na unyama waliofanyiwa na kundi hilo la watu.
Naye
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kitete Dkt.Nassor Kaponta alisema kuwa
wanaendelea kuwapatia huduma katika Hospitali hiyo na hakuna majeruhi
ambaye atahamishiwa kwingine kwa sababu wanauwezo wa kuwasaidia wakiwa
katika eneo hilo hilo.
Aliwataja waliojeruhiwa ni Maria Sahani , Elizabeth Kashindye, Manugwa Lutema na Raheli Mikomangwa. Kabla
ya kufariki marehemu ambaye alikuwa mganga wa kienyeji alikwenda kutoa
matibabu kijiji cha jirani na baada ya kurejesha akaanza kuumwa na
hatimaye usiku wake alifariki kwa sababu ya ugonjwa.
Vitendo
vya kinyama ikiwemo mauaji kwa wanawake Mkoani Tabora vinaanza
kuonekana kama vya kawaida ambapo mapema mwezi Agosti mwaka huu wilayani
Nzega wakinamama watano walipoteza maisha baada ya kushambuliwa na
kisha kuchomwa moto na mwei huo huo wilayani Sikonge mtu mmoja
alinusurika kifo baada ya kufungiwa nyumbani kwake na nyuma kuwekwa moto
0 comments:
Post a Comment