· WAO KUNUFAIKA KWA KILA KOSA KUPATA ELFU 25.
NA TIGANYA VINCENT
RS-TABORA
24 OCTOBER 2017
VIJANA wanaondesha shughuli za usafirishaji wa abiria
kwa njia ya Pikipiki (Boda boda) mkoani Tabora wamepewa jukumu la
kuhakikisha wanasimamia usafi kwa kuwakamata watu wenye tabia za kutupa
takataka ovyo katika maeneo mbalimbali miji na hivyo kuhatarisha afya za watu wengine.
Jukumu hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kanyenye wakati akiwahamasisha
wananchi awamu ya pili zoezi la upandaji miti mingine na usafi wa
mazingira.
Alisema
kuwa kuanzia sasa Boda boda watakuwa wanajukumu la kukamata watu
watakaotupa taka taka za aina yoyote katika mitaa na kwenye maeneo
ambayo hayaruhusiwi na kuwafikisha katika Halmashauri husika.
Mwanri
alisema kila mtu atakayekamatwa kwa kutumia Sheria ndogo ndogo za eneo
husika atalazimika kulipa silingi elfu 50 ambapo kati ya hizo mkamataji
atalipwa shilingi elfu 25 zilizobaki zitakuwa mali ya Halmashauri
husika.
“Ndugu
zangu boda boda leo nawapa mpango mzuri wa kupata pesa ambao ni huu
…ukimwano mtu katupa karatasi ya vocha kamata…ukimwona katupa gunzi
kamata…chupa ya maji kamata na mpeleke Halmashauri kisha atalipa elfu 50
wewe watakupa elfu 25 mnaonaje mpango huo? Aliuza Mwanri .
Alisema
kuwa haiwezekani Tabora ikaendelea kubaki nyuma katika suala la usafi
na viongozi na wananchi wapo ni lazima watu wabadilike na waanze
kuzingatia suala la usafi kwa ajili ya kulinda afya zao na jamii
inayowazunguka.
Alisema
kuwa lengo la mpango huo ni kutaka kuhakikisha Mkoa mzima wa Tabora
unaondokana na aibu ya kuwa na takataka zilizotupwa ovyo na hatime uwe
Mkoa wa kwanza hapa nchini kwa kuzingatia usafi.
Katika
hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amewaagiza viongozi wa Halmashauri zote
kuhakikisha kuwa maduka yote yanayotoa huduma za kuuza vinywaji ,
vibanda vya vyakula na baa ambazo hazina vyoo zinafungwa mara moja.
Alisema
kuwa hakikuta sehemu mtu anayeendesha biashara hiyo huku hana choo
atalazimika kuwachukulia hatua viongozi husika ikiwemo kuwasimamisha
kazi kwa kushindwa kusimamia majukumu yao ikiwemo kulinda afya za
wananchi.
Mwanri
alisema kuwa inapotea tatizo la mlipuko wa magonjwa Serikali inaingia
gharama kubwa kuhakikisha inaokoa maisha ya wananchi kwa hiyo ni vema
kuchukua tahadhari mapema.
Alisema
kuwa hawezi kuvumilia kuona watu wanaendelea kutoa huduma katika
mazingira ambayo sio salama kwa kuwa analojukumu na dhamana ya
kuhakikisha wakazi wote wa Tabora wanakuwa salama na afya bora.
Mmoja
wa Madreva wa Boda boda Bonos Binamungu apongeza hatua ya Mkuu wa Mkoa
kuwakabidhi jukumu la kusimamia usafi na kuahidi kutekeleza jukumu hilo
kwa misingi ya Sheria na taratibu bila kumwonea mtu.
Alisema
kuwa kuondoa mikwaruzano ni vema wananchi wa Tabora wakaanza kutii
sheria ikiwa ni pamoja na kutupa takataka katika maeneo husika ili
kuepuka kupata hasara ya kulipa fedha ambazo hakutarajia.
0 comments:
Post a Comment