NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
21 November 2017.
MWANACHUO mmoja Chuo cha Utumishi wa Umma –Tawi la Tabora kinachojulikana kama Uhazili Raphael Kadesha (22) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia tai ya kuvaa shingoni.
Kwa
mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Graifton Mushi tukio
hilo limetokea leo saa 4 asubuhi ambapo marehemu alifunga tai juu ya
kitanda chake.
Alisema kuwa marehemu alikuwa akisoma kozi cha Cheti cha Awali cha Utawala katika Chuo hicho.
Mushi
aliongeza kuwa chanzo cha kifo hicho hakijulikani na Jeshi la Polisi
linaendelea na uchunguzi kujua nini kilimfanya mwanachuo huyo kuchukua
maamuzi hayo yaliyoacha simanzi katika jamii yake na Chuo kwa ujumla.
Alitoa
wito kwa wanachuoni kuomba ushauri kwa viongozi wao Chuo au wa kiroho
pindi wanapokuwa na matatizo binafisi kwani kujiua sio suluhisho la
matatizo bali ni kuwaongezea walezi wao shida na majonzi zaidi.
Mushi alisema kuwa mwili wa marehemu umehifahiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete.
Naye Mkurugenzi wa Chuo
hicho Dkt. Ramadhani Marijani alitoa wito kwa wanachuo kuwa watulivu
wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa sababu zilizopelekea
mwanachuo huyo kuchukua maamuzi yaliyoacha simamazi sio tu kwa familia
yake bali hata kwa Jumuiya nzima ya Uhazili.
Alisema
kuwa ni vema kama kuna mwanachuo yoyote anakuwa na tatizo au msongo wa
mawazo kuwaeleza viongozi wake wawe wa Serikali ya Wanafunzi, Mama
Mlenzi, Mshauri wa Wanachuo au Mkurugenzi mwenye ili waweze kusaidia
katika ushauri utakaowapa ufumbuzi kuliko kuchukua maamuzi ya haraka.
0 comments:
Post a Comment