NA TIGANYA VINCENT
RS –TABORA
21 NOVEMBA 2017
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora izimetaka Halmashauri zote kuanza mara moja utekelezaji wa agizo la ujenzi na uibuaji wa viwanda visivyopungua 12 katika kipindi mwaka mmoja kuanzia mwezi ujao katika maeneo yao.
Agizo
hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati
akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.
Alisema
kuwa ni vema kila Mkurugenzi Mtendaji anapaswa kukahikisha kuwa anaanza
mara moja utekelezaji wa agizo hilo la ujenzi wa viwanda ili ifikapo
mwishoni mwa mwaka ujao kila eneo liwe na viwanda vipya.
Mwanri alisisitiza kuwa wanatakiwa kuhakikisha kuwepo na viwanda vipya vidogo na vya kati kulingana na maagizo ya viongozi.
Alisema
kuwa hatua itawezesha kusaidia vijana wengi kupata ajira au kujiari
katika viwanda hivyo vitakavyoanzisha na kuwezesha kufikia nchi ya
uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda.
Mwanri
alisema katika kufanikisha dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda,
Maafsia Ugani wote katika kipindi hiki cha msimu wa mvua watakiwa kwenda
vijijini kuwasaidia wakulima ili wawaze kuzalisha malighafi nyingi za
kilimo.
Alisema
kuwa Mkoa wa Tabora unaendelea kusisitiza kilimo cha mazao kama vile
alizeti, mihogo, mpunga, korosho, maembe, karanga kwa ajili ya
upatikanaji wa malighafi za viwandani.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kaliua Revocatus Kuuli alisema tayari wataalamu wake wameshaanza kubainisha viwanda vipya ambavyo wataanzisha katika eneo hilo.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kaliua Revocatus Kuuli alisema tayari wataalamu wake wameshaanza kubainisha viwanda vipya ambavyo wataanzisha katika eneo hilo.
Alisema kuwa kwa upande wao wanatarajia kuvuka lengo na kuwa na viwanda vingi ambavyo vitasaidia kutoa ajira kwa vijana wa eneo.
0 comments:
Post a Comment