Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax
Mutagwa (kulia), akimkabidhi mbegu ya mahindi aina ya Wema, Mkuu wa
Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, Peres Boniface Magiri wakati
wa uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109, mihogo na
viazi lishe kwa ajili ya mashamba darasa katika vijiji vya Isunda,
Kisanga, Udongo na Kanyamsenga wilayani humo jana.
Wanakikundi cha Aliselema wakishusha mbegu ya mihogo tayari uzinduzi wa shamba darasa.
Ofisa
Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza
kabla ya kuanza uzinduzi huo katika Kijiji cha Isunda kilichopo Kata ya
Nkolye.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Pares Magiri akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Isunda.
Wanakikundi cha Aliselema wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mtafiti
wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku
kilichopo mkoani Kagera Jojianas Kibura akielekeza namna ya kupanda
mihogo.
Mtafiti
wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku
kilichopo mkoani Kagera Jojianas Kibura akimuelekeza namna ya kupanda
mbegu ya mihogo mkuu wa wilaya hiyo.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Aliselema, Amir Hassan akipanda mbegu ya mihogo.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa akipanda mbegu ya mihogo katika shamba darasa.
Mwenyekiti
wa Kikundi cha Aliselema, Amir Hassan akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu changamoto waliyokuwa nayo ya kupata mazao kiduchu kwa
kutumia mbegu zisiso bora.
Wakulima wakisubiri kuelekezwa namna ya upandaji wa mbegu hizo za mihogo.
Mkuu
wa Wilaya ya Sikonge, Pares Magiri akizungumza na wakulima wa Kijiji
cha Kisanga kabla ya uzinduzi wa shamba darasa la viazilishe.
Mtafiti
wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku
kilichopo mkoani Kagera Jojianas Kibura akimuelekeza namna ya kupanda
mbegu ya viazilishe katika kijiji cha Kisanga.
Wanawake wa Kijiji cha Kisanga wakiwa kwenye uzinduzi huo wa shamba darasa la mbegu ya viazilishe.
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru mkoani Mwanza, Mariana akielekeza namna ya upandaji wa viazilishe.
Mkuu wa Wilaya, Peres Magiri akipanda mbegu ya viazilishe wakati wa uzinduzi wa shamba hilo.
Mwalimu wa Baraka Kita wa Shule ya Msingi Sogea B, akipanda mbegu hiyo ya viazilishe.
Mkulima, Mariam Said akipanda mbegu ya viazilishe
Mwalimu George Adamu Mwalwizi, akizungumzia mbegu mpya ya viazi lishe walioletewa kuwa itakuwa ni mkombozi kwao na wanafunzi.
Na Dotto Mwaibale, Sikonge Tabora
WANAFUNZI
wilayani Sikonge mkoani Tabora wataanza kunufaika na viazi lishe baada
ya kupokea mbegu bora ya viazi hivyo, mihogo na mahindi ya Wema kutoka
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na
Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)
Hayo
yameelezwa katika Kijiji cha Kisanga na Mkuu wa Wilaya hiyo, Peres
Boniface Magiri wakati akizungumza na wakulima kwenye uzinduzi na
kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109, mihogo na viazilishe kwa
ajili ya mashamba darasa katika vijiji vya Isunda, Kisanga, Udongo na
Kanyamsenga.
Magiri
alisema baada ya kuotesha mbegu hiyo ya viazilishe kwa wingi
kitakachofuata ni kuanzisha utaratibu wa wanafunzi katika shule
mbalimbali za wilaya hiyo kupata chakula cha mchana badala ya kwenda
nyumbani.
Alisema
wilaya hiyo kupelekewa mbegu hizo kwao ni fursa kubwa na kwa
kushirikiana na wakulima na maofisa ugani atahakikisha mashamba darasa
hayo yanatunzwa na kutoa mrejesho.
Aliongeza
kuwa shule mbalimbali zitaanzisha mashamba ya viazilishe hivyo ili
kumaliza tatizo la kukosa chakula kama sio kulipunguza.
"Tunahitaji
matokeo chanya ya mashamba darasa hayo yawasaidie wakulima wengine
katika wilaya hiyo na kuwa atahakikisha anatembelea mara kwa mara yalipo
mashamba hayo" alisema Magiri.
Mtafiti
wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku
kilichopo mkoani Kagera Jojianas Kibura aliwaambia wakulima kuwa hekta
moja ya muhogo kwa kutumia mbegu hiyo bora inaweza kutoa tani 25 hadi 32
wakati viazi itatoa tani 7 hadi 9 kwa Hekta moja.
Alisema
kuwa endapo watafuata kanuni bora za kilimo cha mazao hayo kwa
kuzingatia nafasi kati ya mche na mche na mstari kwa mstari na matumizi
ya mbolea wataweza kuongeza uzalishaji zaidi tofauti na sasa ambapo
kwenye hekta moja ya muhogo wanapata tani nane hadi kumi wakati kwenye
viazi wanapata tani moja hadi 3.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax
Mutagwa, alisema mbegu hiyo ya mahindi imefanyiwa utafiti na inavumilia
ukame wakati ile ya mihogo ikivumilia magonjwa kama batobato na
michirizi kahawia huku zikitoa mavuno mengi.
0 comments:
Post a Comment