Home » » ELIMU YA MATUMIZI YA NISHATI MBADALA KUNUSURU MAZINGIRA

ELIMU YA MATUMIZI YA NISHATI MBADALA KUNUSURU MAZINGIRA

WANANCHI waishio maeneo ya Vijijini endapo watapata elimu kuhusu matumizi ya Nishati mbadala,watakuwa katika nafasi nzuri ya kutunza mazingira yanayoharibiwa kwa kasi kutokana na matumizi ya kuni katika kukaushia tumbaku na matumizi ya Nyumbani. Akifungua mafunzo kwa walimu wa Umeme Vijijini wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii,Mkuu wa Wilaya ya Uyui,Bi Lucy Mayenga katika Hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala,Bw.Bibangamba John,ameeleza ni lazima elimu ya matumizi sahihi ya Nishati mbadala itolewe ili wananchi wasizidi kuharibu mazingira. Ameeleza wananchi wanatumia sana kuni na kuharibu mazingira lakini matumizi ya Nishati mbadala yatawasaidia sana kuokoa na kutunza mazingira ambayo ni muhimu kwa ustawi wa maisha yao. Mayenga amesisitiza kwa wshiriki hao kuhakikisha kweli wanaipeleka elimu hiyo kwa wananchi wengi waishio vijijini vinginevyo itakuwa ni kazi bure. Kwa upande wake Afisa Kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na watoto,Pius ligo,amesema Wakala wa Nishati Vijijini,REA, wanataka wananchi wasitumie Nishati inayoharibu mazingira. Amesema mafunzo hayo yanayotolewa kwa washiriki kutoka Mikoa Tisa Nchini yatatumika kueneza elimu ya matumizi ya Nishati mbadala kwa wananchi wa Vijijini kupitia washiriki hao na hivyo kuleta ustawi wa maisha ya wengi Mafunzo hayo yanayochukua Wiki mbili yanayoendeshwa na wakala wa Nishati Vijijini,REA kwa kushirikiana na Wizara ya maendeleo ya Jamii,yatawapeleka washiriki kufunga Nishati katika zahanati ya Miyenze ambayo itakuwa ni sehemu ya mafunzo yao.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa