Home » » WATAKA SHERIA YA ZAMANI YA MANUNUZI IFUTWE HARAKA

WATAKA SHERIA YA ZAMANI YA MANUNUZI IFUTWE HARAKA

Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2011 yatakiwa kuanza kutumika
SHERIA ya manunuzi ya mwaka 2004 imeelezwa kuwa inatakiwa iachwe kutumiwa na badala yake ile ya mwaka 2011 ianze kutumika haraka kwani ina manufaa makubwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tabora,Uyui,Mh Said Ntahondi amesema sheria ya mwaka 2004 ina mapungufu yanayopelekea pesa nyingi kutumika katika miradi ya maendeleo huku mchakato wake ukiwa ni mrefu pesa ambazo zingeweza kukokolewa na kutumika katika shughuli zingine za maendeleo
Akizungumzia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi Makao makuu ya wilaya ya Uyui,Isikizya,Mwenyekiti huyo amesema sheria ya manunuzi ya mwaka 2011 ina manufaa makubwa ukilinganisha na ile ya mwaka 2004.
Mheshimiwa Ntahondi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ilolangulu,amesema kwa kutumia njia ya manunuzi ya moja kwa moja badala ya mkandarasi wameokoa zaidi ya asilimia Arobaini ya gharama za ujenzi wa kituo cha Polisi kwani kilikuwa kitumie shilingi zaidi ya Milioni Mia tatu lakini kwa kutumia manunuzi ya moja kwa moja wameokoa zaidi ya shilingi Milioni Mia Moja na Hamsini. Halmashauri ya wilaya ya Tabora,Uyui imejipanga kupiga hatua kimaendeleo na kuboresha Makao yake makuu kwa majengo yenye ubora unaokubalika.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa