WATOA huduma ngazi ya
jamii wanaoshughulika kuzuia vifo vya akinamama na watoto wilayani Sikonge
wametakiwa kufanya kazi zao kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili lengo la
kukokoa vifo vinavyozuilika lifikiwe.
Akizungumza na watoa
huduma hao wakati wa makabidhiano ya Baiskeli zilizotolewa na shirika la CARE
kupitia mradi wake wa Tabasamu,Mkuu wa wilaya ya Sikonge,Bi Hanifa Selengu
amewataka pia kujiepusha na vishawishi katika kazi yao.
Wakizungumzia malengo
ya Mradi huo,Afisa wa CARE ,Bw.Waziri Rashid,amesema ni kuokoa maisha ya
wanawake na watoto na kuongeza matumizi ya njia za uzazi wa mpango.
Nao watoa huduma
ngazi ya jamii wakiongozwa na Bw.Mario Venance,wametaka ushirikiano kutoka kwa
jamii ili kupunguza vifo vya akinamama na watoto vinavyoweza kuzuilika.
Mradi wa Tabasamu wa
Shirika la CARE unatoa mafunzo kwa watoa huduma ngazi ya jamii kabla ya kuanza
kufanya kazi huku ukiwa na lengo la kupunguza vifo vya akinamama na watoto
ambapo watafikiwa laki moja na elfu themanini na sita, wilayani Sikonge.
0 comments:
Post a Comment