Home » » MIL. 40/- ZAIDHINISHWA UYUI

MIL. 40/- ZAIDHINISHWA UYUI


JIBU LA SWALI LA MBUNGE Tabora kaskazini

na Mwandishi wetu, Dodoma
SERIKALI imesema katika kipindi cha mwaka uliopita wa fedha, Halmashauri ya Wilaya ya Uyui ilitenga na kuidhinisha shilingi milioni 40 ambazo zilitumika kupima ubora wa maji katika chemchemi ya Kijiji cha Isikizya na kubaini kuwa maji haya yanafaa kwa matumizi ya binadamu.
Hayo yalielezwa mjini hapa jana na Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia elimu, Kasim Majaliwa, wakati alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM).
“Fedha hizo zilitumika kupima ubora wa maji katika chemchemi ya  Kijiji cha Isikizya na kubaini kuwa maji haya yanafaa kwa matumizi ya binadamu,” alisema Majaliwa.
Katika swali lake la msingi, mbunge huyo alihoji kwa nini serikali isiyatambue maeneo ya Tabora Kaskazini ambayo yanapatikana chemchemi ya maji kama yanafaa kwa matumizi ya binadamu, kisha kuboresha huduma hiyo.
“Katika Kata ya Magiri na Ishihimulwa na maeneo ya Tabora Kaskazini, kunapatikana maji ya chemchemi, kwanini serikali isiyatambue? ” alihoji mbunge huyo.
Alifafanua kuwa, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2011/12, kiasi cha shilingi milioni tisa kutoka katika mapato ya halmashauri, zimetumika kupima ubora wa maji katika chemchemi za Ilolangula, Mabama, Upunge, Magiro na Ufuluma katika Jimbo la Tabora Kaskazini na kubaini kuwa maji haya yanafaa kwa matumizi ya binadamu.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa