Home » » ‘Msisingizie wachawi baada ya kupata magonjwa’

‘Msisingizie wachawi baada ya kupata magonjwa’

WAZAZI Mkoani Tabora wametakiwa kuachana na dhana potofu kuwa watoto wao wanapoumwa wanakuwa wamerogwa.

Mkuu wa mkoa wa Tabora katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa wilaya ya Tabora,Bw.suleiman kumchaya,ameeleza wapo wazazi watoto wao wanapoumwa hudhani wamerogwa na kukimbilia kwa waganaga wa kienyeji.

Amesema magonjwa wanayodhani watoto wao wamerogwa huwa ni magonjwa yanayoweza kuzuilika kupitia chanjo na kuwataka wazazi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hasa kipindi hiki cha wiki ya chanjo Kitaifa.

Kwa upande wake kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Dk Paschal Nyango,amesema chanjo mbalimbali zitatolewa kwa watoto walio chini ya mwaka mmoja zikiwemo za pepopunda,polio na kifua Kikuu.

Amesema watoto zaidi ya laki moja na Elfu Ishirini wanatarajiwa kupatiwa chanjo za aina mbalimbali Mkoani Tabora.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa