MFUKO wa Pesheni kwa watumishi wa umma
(PSPF) Mkoani Tabora, umetoa tuzo ya Taaluma kwa wanachuo watatu wa Chuo
cha Ualimu Tabora, waliofanya vyema kwenye mitihani yao kwa mwaka 2012/2013.
Afisa Mfawidhi wa PSPF Peter Rushaki
amesema PSPF imeanzisha huduma mpya ya utoaji tuzo za kitaaluma kwa
waalimu watarajiwa, ambazo zitakuwa zikitolewa kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho
kwenye vyuo vya ualimu, ambapo chuo cha Ualimu Tabora kimepewa kipaumbele.
Amesema lengo ni kutoa motisha na
kuinua kiwango cha elimu kwa walimu watarajiwa waliopo Vyuoni.
Waliozawadiwa kwa kufanya vizuri ni
Michael Charles aliyezawadiwa shilingi Laki tatu kwa kuwa mshindi wa kwanza,
Ayoub Kibamba,mshindi wa pili alizawadiwa shilingi Laki Mbili na Joyce Kipeta
aliyepata shilingi laki moja kwa kuwa mshindi wa tatu.
Akizungumza kwenye halfa hiyo, Mkuu wa
Chuo cha Ualimu Tabora, Sister Agnes Awaki, ameishukuru PSPF kwa hatua
waliyofikia na kwamba yeye na wanachuo wana imani kubwa sana na mfuko huo
akisema amefurahiswa na hatua hiyo na kwamba kila mara amekuwa akiwasisitiza
wanachuo kusoma kwa bidii na angependa kuona wanaweka jitihada zaidi kwenye
masomo.
Naye Michael Charles, mwanachuo
aliyepata zawadi ya kwanza ya shilingi Laki tatu, akizungumza kwa niaba ya
wenzake, ameishukuru PSPF kwa jitihada zao za kuwajali wanachuo na
kwa uamuzi wao wa kuweka tuzo hiyo ya kitaaluma kwa walimu watarajiwa kwani ni
hamasa kwa walimu kujiunga na mfuko huo.
0 comments:
Post a Comment