WAKATI Sekondari Nyingi
za Kata Nchini zikiwa hazina majengo ya maabara na kama yapo
hayajakamilika,Sekondari ya Kata ya Kazaroho tayari imeanza kutumia majengo
yake ya maabara na mwaka huu wanafunzi wake wa kidato cha nne watafanya Mtihani
wa Kitaifa kwa vitendo.
Hatua hiyo inaweka
matumaini kwa wanafunzi wa shule hiyo wengi wao sasa kuanza kusoma masomo ya
Sayansi na kuamini Shule za Kata zitakuwa mkombozi kwa wanafunzi na jamii kwa
ujumla ikiwa zitapewa msaada zaidi.
Akizungumzia hali
hiyo,Mkuu wa Shule hiyo,Mwalimu George Ndaki,amesema ana matumaini shule yake
itafanya vizuri,akiongeza shule za Kata zisibezwe kwani zina uwezo wa kutoa
wataalamu watakaolisaidia Taifa.
Diwani wa Kata ya
Kazaroho,Mh Haruna Kasele,amebainisha kuwa tayari wameanza kuona matunda ya
sekondari za Kata kwa wanafunzi wake watano kujiunga na Chuo Kikuu mwaka jana
huku lengo lao likiwa ni kuinua Elimu kwenye Kata ya Kazaroho.
Diwani Kasele amesema
sasa msisitizo utakuwa ni kuwahimiza wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa
vile Maabara na madawa yapo ili wapatikane wanasayansi wa fani mbalimbali
watakaolisaidia Taifa
Shule hiyo ya Kazaroho
ni mojawapo ya shule tatu za Halmashauri ya wilaya ya Urambo yenye Wilaya mbili
za Urambo na Kaliua ambazo majengo yake ya maabara yamekamilika na yanatumika.
0 comments:
Post a Comment