MAJAJI wa Mahakama ya Rufaa Nchini wanaoendelea na kikao
mjini Tabora wametupilia mbali Rufaa tatu zilizofunguliwa kupinga
maamuzi yaliyotolewa na Mahakama za chini kwamba hayakuwa sahihi kuwatia
hatiani.
Rufaa zilizotupwa ni yenye namba 455/2007 iliyofunguliwa na
Kija Nestory akipinga adhabu ya kifo aliyopewa baada ya kutiwa hatiani kwa
mauaji ya watu watatu na wizi wa ngombe zaidi ya Hamsini.
Katika Rufaa hiyo Kija alipinga adhabu hiyo huku akidai
kwamba ushahidi uliotolewa dhidi yake ukiwemo wa utambuzi haukuweza
kutosheleza na kuthibitisha yeye kutiwa hatiani kama ilivyoamuriwa.
Awali katika kesi ya msingi ilidaiwa kwamba tarehe 20 Agosti
1999 katika kijiji cha Mwangali Mkoani Shinyanga mrufani
aliwaua Masigana Nundu, Nsamaka Jilala na Ngwalu Chele.
Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufaa chini ya uenyekiti wa
Jaji Nathalia Kimaro, Jaji William Mandia na Jaji Simon Kaijage pia limetupilia
mbali rufaa ya Masima Mohamed aliyetiwa hatiani kwa kosa la ubakaji.
Akisoma maamuzi ya rufaa hizo kwa niaba ya Majaji hao Kaimu
Msajili wa Mahakama hiyo Maximillian Malewo, Alisema kuwa waliosikiliza
shauri hilo lililokuwa
na mashitaka mawili aliyoyatenda 19 Novemba 2003 walithibitisha
makosa dhidi ya mrufani pasipo shaka yoyote.
0 comments:
Post a Comment