Home » » Walimu wakwamisha maendeleo ya SACCOS

Walimu wakwamisha maendeleo ya SACCOS


BAADHI ya Vyama vya kuweka na kukopa  ,SACCOS ,Mkoani Tabora vinakabiliwa kuwa katika hali mbaya kifedha kutokana na makato ya mikopo ya walimu kutowasilishwa katika SACCOS hizo.

Katibu wa chama cha walimu Mkoani Tabora, Bi Romana Alloys,amesema makato ya walimu hayawasilishwi katika vyama hivyo na kuviweka katika hatari ya kufa.

Akisoma risala katika uzinduzi wa Jengo la walimu Mkoani Tabora,Katibu huyo amezitaka halmashauri zote kutoa ushirikiano wa kutosha kwa SACCOS hizo ili ziendelee kuwahudumia wanachama wao.

Amezitaja changamoto zinazowakabili walimu kuwa ni nyingi lakini kazitaja baadhi kuwa Halmashauri nyingi kuchelewesha upandishaji madaraja ya walimu sanjali na Vyeo

Bi Romana  amesema tangu CWT ianze jitihada zake za kuwatetea waalimu  hapa nchini  mnamo mwaka 1993, wamepata mafanikio makubwa ikiwemo kuwaunganisha waalimu wote na  kutambuliwa na serikali na kujenga majengo ya vitega uchumi katika mikoa yote hapa nchini, jitihada ambazo zinaendelea mpaka sasa.

Jengo hilo la kitega uchumi lenye Gorofa mbili limejengwa na kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT kwa gharama ya shilingi Milioni 347.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa